Here are the lyrics of Nani Kama Wewe by Gloria Muliro featuring Man Ingwe and Mercy Linah.
Ni nani kama wewe x3
Mungu mkuu (Repeat)
Kwa neno lako Bwana
Uliumba dunia na vyote vilivyomo
Jina lako Baba, limeinuliwa juu ya yote
Hakuna, hakuna kama wewe
(Refrain)
Uinuwae wanyonge
Wawaketisha na wafalme
Hakuna uwezaye tenda ila wewe
Nikitazama maisha yangu
Ulikonitoa Yesu wangu
Nina sababu ya kusema, ni wewe pekee
(Refrain)
Nani mwenye uwezo
Nani mwenye rehema tele
Nani mwenye enzi kama yako
Ni wewe pekee
Wastahili sifa zote
Mbinguni na duniani Baba
Twakusujudu, twakuabudu, twakuheshimu
(Refrain)
Umetukuka adonai, el shadai
Mungu mwenye nguvu
Ni nani mwingine kama wewe
Hakuna wa kulinganishwa na wewe Baba
Nani kama wewe Baba/Yahweh