KAMBUA
BADO NASIMAMA
CHORUS
Bado nasimama, bado naendelea.
Bado najikaza, nifike kule.
Bila neema na rehema Zako
Ningekuwa wapi mimi?
Bila upendo na fadhili Zako
Maisha yangu yangekuwa bure
Kwa wema Wako kanisimamisha
Na imani yangu Ukaiweka salama
Kama si Wewe mwamba wa wokovu wangu
Nisingeweza, ningeangamia
CHORUS
Bado nasimama, bado naendelea.
Bado najikaza, nifike kule.
Nainua macho yangu
Kwako wewe, Baba yangu
Msaada wangu utatoka wapi
Msaada wangu u katika Bwana
Hasinzii anilindaye
Hanianchi mimi niteleze
Anipa nguvu na uwezo Wake
Ili mimi nifike kule
Nifike kule